Category: slides

TANGAZO LA USAJILI

 

Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) ni Mamlaka yenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya tasnia ya nyama, iliyoanzishwa kwa Sheria ya Nyama No. 10 ya Mwaka 2006. Kifungu Na. 17 (1) cha sheria hii, kinazuia mtu yeyote kufanya shughuli ya aina yoyote katika tasnia ya nyama bila ya kuwa na cheti cha usajili kutoka Bodi ya Nyama Tanzania.

Bodi ya Nyama Tanzania, ina watangazia wadau wote wa tasnia ya nyama kusajili ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. Tangazo hili linawalenga wadau wote wa tasnia ya nyama ikiwa ni pamoja na:

 1. Wafugaji wa mifugo ya aina zote inayozalisha nyama;
 2. Wafanyabiashara wa Mifugo;
 3. Wasafirishaji wa mifugo na nyama;
 4. Wenye machinjio za aina zote;
 5. Wenye bucha za kuuza nyama za aina zote;
 6. Wasindikaji wa nyama
 7. Supermarket na duka la bucha
 8. Wasambazaji wa bidhaa za nyama;
 9. Waingizaji wa nyama nchini;
 10. Wasafirishaji wa mifugo, nyama na bidhaa zake nje ya nchi;
 11. Waendesha matamasha ya nyama choma.

Kwa sasa usajili unatolewa katika Ofisi za Bodi zilizopo ndani ya majengo ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Veterinari Complex, 131 Barabara ya Nelson Mandela, 15487 Dar es Salaam, au wasilianana Msajili wa Bodi, S.L.P 6085, Dar es salaam, simu +255 713 412756, barua pepe info@tmb.or.tz. Tembelea Tovuti yetu www.tmb.or.tz kwa maelezo zaidi na kupata fomu za kuomba usajili.

Bodiya Nyama Tanzania itafanya ukaguzi wa shughuli za biashara za wadau wa tasnia ya nyama wakati wowote kuanzia mwezi Februari, 2016. Mdau atakayekutwa akifanya shughuli za biashara katika tasnia ya nyama bila kusajili anatenda kosa na akikutwa na hatia atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupoteza sifa za kufanyabiashara hiyo (kufungiwa biashara).

WAHI SAJILI SASA

Quality and Safe Meat

Picture4

Language :Kiswahili